Daddy! Diamond Apeleka Watoto, Zari Uwanja Wa Ndege Baada Ya Kukaa Siku 5 TZ

zari na diamond
zari na diamond

Zari na watoto wake wawili, Princess Tiffah na Prince Nillan, wamerudi Afrika Kusini. Walitumia siku tano nchini Tanzania na walikuwa wakikaa katika MJENGO ya Diamond Platnumz.

Zari au The Boss LADY, alikuwa katika nchini Tanzania alipata kufanya matukio kadhaa ikiwa ni pamoja na kuchangia taulo za usafi kwa wasichana wanafunzi na kuhudhuria kikao cha bunge mjini Dodoma baada ya kutajwa kuwa balozi wa utalii Tanzania.

Siku ya Jumapili mchana, Diamond, mama yake na babake wa kambo walimsindikiza Zari pamoja na watoto wake wawili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na walipiga picha pamoja. Wote walionekana kuwa na furaha.

Diamond na Zari wanashirikiana kulea watoto, na wengi wanaamini kwamba wanajari kurudisha mahusiano yao yaliyo anguka miaka kadhaa iliyo pita. Wapenzi hao wawili wa zamani wanatengeneza pesa kutoka makampusi makubwa Afrika, pia watoto wao wawili, nao ni mabalozi wa brands wa akaunti za benki na maduka ya mavazi kwa watoto.

Kua wa kwanza kupata taarifa

You may also like...