Gift Stanford ‘Gigy Money’ Mrembo Machachari Mwenye Sura Mbili

Gift Stanfor Gigy Money
Gift Stanfor Gigy Money

Jina Gift Stanford, Ni jina zuri sana na lina nguvu sana, ukilitamka utajua tu mwenye jina hili ni mtu flani mashuhuri. Ni kweli, mwenye jina hili ni mashuhuri kweli kweli; Ila tu nadhani kwa kuogopa ukubwa na heshima ya jina hilo; kaamua kujibatiza jina lisilo na uzito uliobeba wazazi, ndugu jamaa na marafiki. Huyu ni Gigy Money. Kama hafungua kinywa chake kuongea usipoambiwa huyu ndio Gigy Money huwezi kukubari, ni msichana mrembo mwenye mvuto na haiba.

Gift Stanford 'Gigy Money'
Gift Stanford ‘Gigy Money’ katika pozi la utulivu.

GIFT – @GigiMoney: Jina hili linambeba kama demu msela sana, Mwana sana, Hustler, Demu wa kigheto deep, msaka tonge, kudanga sio tatizo, mwanamziki, ngumi knononi na mengine mengi; kiasi kwamba ukimtafuta google kwa kutumia gigymoney, basi utakutana na mchanganyiko wa habari zenye matukio lukuki. Ikichanganyikana na nyimbo zake kadhaa. Huyu ndio Gigy money kama gigymoney.

Gigymoney kama Gift Stanford: Ukitafuta kwenye mitandao na google; hutapata kitu, na hata ukipata ni vitu vya kawaida kama binadamu wa kawaida mwenye maisha ya kawaida. Ambapo Gift kama Gift anabaki kuwa ni Gift, ni Mama, ni Mwanamziki. Ni jina ambalo amelitunza vizuri sana na nina hakika bado lina heshima kubwa sana kwenye jamii hata kwenye familia yake.

Naweza mshauri binti huyu, japo si nafasi yangu; lakini naongea kama kaka, mjomba, jirani ama kama mwandishi; Mpaka alipofika; anaweza kugeuza maisha na bado akaishi vizuri na kwa uhuru, Jina gigymoney limemtoa mbali na limempeleka mbali lakini jina hilo linamfanya aishi maisha kwa ugumu sana. Kwa hatua aliyo nayona connections alizonazo anaweza kuishi na kutengeneza pesa nzuri kumtosha yeye na mtoto wake hata kutimiza ndoto za maisha yake.

UPDATE: 7 May 2021: Katibu mkuu wa Chama Cha Muziki Wa Kizazi Kipya Tanzania Samweli Mbwana, amesema wameandika barua kwenda BASATA kuwataka kumwachia Msanii GigiMoney.

January 5 Msanii GigyMOney alihukumiwa na BASATA kutojihusisha na mzik/sanaa kwa kipindi cha miezi sita na kupigwa faini ya Tsh Milioni moja.

You may also like...