Howard University Kubadili Jina La Chuo Chake Cha Sanaa; Kutumia Jina La Chadwick Boseman

howard university Chadwick boseman
howard university Chadwick boseman

Chuo Kikuu cha Howard(Howard University) kinabadili jina Chuo cha Sanaa baada ya mwanafunzi wa zamani Chadwick Boseman. Rais wa Chuo Kikuu, Wayne A. I. Frederick alitangaza Jumatano, akisema Chuo cha Sanaa kilichoanzishwa upya kitaitwa kwa heshima ya mwanafunzi wa zamani Chadwick Boseman.

“Katika kipindi chake hapa Howard, Boseman aliongoza maandamano ya wanafunzi dhidi ya uingizwaji wa Chuo cha Sanaa katika Chuo cha Sanaa na Sayansi. Muda mrefu baada ya kuhitimu, yeye, pamoja na wanachuo wengine, waliendelea kufanya mazungumzo na uongozi wa Chuo Kikuu cha Howard – juhudi zao hazikuwa za bure. Mipango ya kuanzisha tena Chuo cha Sanaa ilitangazwa mapema mwaka 2018, ”Chuo Kikuu kimesema.

Katika taarifa hiyo, mke wa Chadwick, Simone Ledward-Boseman, alisema;

Nimefurahi sana kwamba Chuo Kikuu cha Howard kimechagua kumheshimu mume wangu kwa njia hii na kwamba Bi Rashad amekubali jukumu la kua Mkuu wa Chuo hiki, – wote Howard na Bi Rashad walichangia sehemu muhimu katika safari yake kama msanii. Kuanzishwa tena kwa Chuo cha Sanaa katika jina la Chad, itasaidia vizazi vijavyo kueleza hadithi ya maisha ya chad na kuhakikisha kuwa urithi wake utaendelea kuhamasisha waandishi wa hadithi vijana kwa miaka ijayo.

mke wa Chadwick, Simone Ledward-Boseman

Pia, mwigizaji wa Kimarekani Phylicia Rashad (NBC’s “This Is Us”, Fox TV Series “Dola”, “Soul”) amechukua jukumu la kua Mkuu wa Chuo hicho cha Sanaa cha Howard.

Phylicia Rashad

Akizungumzia majukumu lake jipya, alisema, “Ni bahati kubwa kutumikia katika nafasi hii na kufanya kazi na uongozi wa Chuo Kikuu cha Howard, kitivo na wanafunzi katika kuanzisha tena Chuo cha Sanaa.”

Akimpongeza Phylicia juu ya mafanikio yake na jukumu lake jipya, Rais wa Chuo Kikuu Cha Howard, alisema kwamba hangeweza kufikiria mtu mwingine yeyote “kuchukua jukumu hili kuliko Bi Phylicia Rashad. Tunapoanzisha tena jamii yetu ya vyuo vikuu na ulimwengu kwa jumla kwa Chuo cha Sanaa cha Howard, mkuu huyu mpya(Phylicia Rashad) atachukua jukumu muhimu katika kuhakikisha mwanzo mzuri wa taasisi hii iliyoanzishwa tena. “

“Kwa kuzingatia sifa ya Bi Rashad pamoja na uwezo wake na orodha ya kuvutia ya mafanikio, bila shaka atakipa chuo hiki uwezo wa kuvuka hata matarajio yetu makubwa. Chini ya uongozi wake, Howard itaendelea kuhamasisha na kukuza wasanii na viongozi ambao wataunda tamaduni zetu za kitaifa kwa vizazi vijavyo. “

Kua wa kwanza kupata taarifa

You may also like...