Jack Cliff Atoka Jela Baada ya Kutumikia Kifungo China

Jack Cliff Atoka Jela Baada ya Kutumikia Kifungo China
Jack Cliff Atoka Jela Baada ya Kutumikia Kifungo China

Hatimaye model maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Cliff’ ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka nane jela Macao nchini China ambapo alikuwa akitumikia kifungo chake tangu tangu mwaka 2014 kutokana na kosa la kutaka kuingiza dawa za kulevya mjini Macao mwezi Disemba 2013.

Jackie amethibitisha hilo usiku wa kuamkia leo Novemba 16, 2021 baada ya kupost kwenye page yake mpya kwenye Instagram @ms.jackiecliff

TUJIKUMBUSHE

Jackie alikamatwa Desemba 19, 2013 akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.

You may also like...