TGNP YASIKITISHWA NA KITENDO CHA KUTOLEWA NJE YA BUNGE KWA MBUNGE CONDESTER SICHWALE

TGNP yasikitishwa gozeep
TGNP yasikitishwa gozeep

Taasisi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP imesikitishwa na kitendo cha kutolewa  nje  kwa  mbunge wa Momba Condester Sichwale kwa madai ya kuvaa mavazi yaliyo kinyume na Kanuni na Taratibu za Bunge.

TGNP Mtandao imesema kitendo  hicho ni cha kumdhalilisha mbunge huyo ambaye ni  kioo  na hamasa kwa wanawake wengi viongozi na wenye nia ya  kuwa  viongozi.

Akizungumzia tukio hilo mkurugenzi mtendaji wa  TGNP   amesema wanaamini  kuwa  bunge  linaongozwa  na Kanuni  na  Sheria  ambazo  zimebainishwa  wazi  namna  ya  kuwajibisha  wabunge  ambao  watakiuka  kanuni na  sheria  hizo, ikiwemo  Spika  kujiridhisha kumtoa  nje  Mbunge kama  ilivyoelezwa  katika  ibara  ya 149 ya  kanuni  za kudumu  za Bunge.

Kwa  upande  wake  afisa Programu  TGNP  Jackson  Malangalila kwa  upande amesema  kupitia  kitendo  cha  mbunge  Sichwale  kuondolewa  bungeni  kwa  sababu  ya  madai  ya  mavazi  inaonyesha  ni  tendo linalo endelea   kukandamiza  nafasi  ya mwanamke .

Aidha TGNP imetoa wito kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania  akiwa ni kiongozi  wa Bunge kutumia busara na hekima na kuzingatia kanuni  katika  kukabiliana na matukio kama  hayo  bungeni ili  kuhakikisha  haki  na  usawa  vinasimamiwa na kuzingatiwa  bungeni kwa manufaa mapana  ya  taifa.

Ikumbukwe kuwa mbunge wa Momba Condester Sichwale (CCM) jana alitolewa bungeni  kwa madai ya kuvaa mavazi yasiyo na staha katika Bunge hilo.

Tayari baadhi ya wabunge wameonekana kuchukizwa na kitendo hicho akiwemo mbunge wa Nyasa Mhandisi Stela Manyanya na Jacklin Ngonyani waliomba muongozo wa spika kwa madai mbunge aliyetolewa nje alionewa.

Kua wa kwanza kupata taarifa

You may also like...