Wana Twita ‘Wanaompinga’ Diamond Platnumz BET2021- Ni Chuki Binafsi

Diamond Platnums for bet2021
Diamond Platnums for bet2021

Karibu wiki mbili sasa kutembelea twita kumekua na ukakasi usiovumilika, kuona Mtanzania akimtakia mabaya Mtanzania mwenzake. Watu wa Taifa moja wakioneana hila na kutaka mmoja asipate ama kupiga hatua flani. Hii inakua baada ya msanii kutoka Tanzania kuingia kwenye orodha ya wasanii kadhaa walio chaguliwa kuingia katika kuwania tuzo ya BET, habari yake iliandikwa hapa >> Diamond Platnumz Anawania Tuzo Ya ‘Best Internationa Act BET 2021’ Peke Yake E. Africa, S. Africa na baadae watu wengi na baadhi ya taasisi mbalimbali walitoa pongezi zao hasa tu kwa Diamond Platnumz kutokea katika kinyang’anyiro hicho, na moja ya taasisi hizo ni COSOTA ambaya ni Taasisi ya Haki Miliki Tanzania; COSOTA: Diamond Platinumz Kuwania Tuzo BET Ni Heshima Kwa Taifa Na Sanaa Ya Muziki Wa Bongo Fleva. Mtu anapo fanya vyema ni jambo la busara sana kumpongeza hata kumuunga mkono bila kujarili tofauti zenu kiitikadi za kisiasa, imani hata ukabila au utaifa ama. Wanasiasa wengi baada ya uchaguzi hutakiana heri na kuungana kwa maslahi mapana.

Hii imekua tofauti sana kwa wasanii na baadhi ya watu hasa huko katika ulimwengu wa twitter, Kijana mpambanaji aliye dhihirisha kua kweli hapendi umaskini, Diamond Platnumz akishikwa shati na watu wachache ambao wameshindwa kua na vifua vipana kuficha chuki zao na kuweka utaifa kwanza. Hii ni akili fupi kabisa na inadhihilisha kua hawajachukua muda kufikiria madhara yake si kwa diamond platnumz pekee bali hata kwao. Upande wa diaxamond platnumz, si kwamba hawezi kuishi bila BETAwards, hata kabla ya BET tayari ana maisha yake na misingi yake kimuziki na nje ya mziki. Ila kwa diamond kupata ama kua katika orodha hiyo tu, kunamuongezea CV na kufungua milango zaidi kwake kukua na kadiri anavyo zidi kukua pia anazidi kupanuka kibiashara na anavyo zidi kupanuka kibiashara atazidi kuajiri ama kutengeneza ajira zaidi kwa Watanzania na wengine. Nina hakika tunakokwenda hao hao wanao ongea kama sio wao basi watoto wao watakuja ajiriliwa na jasho la huyu huyu tunae mbeza leo.

Nenda Wasafi Radio sasa hivi uliza mtangazaji yoyote kama miaka kumi iliyopita angeambiwa kua miaka kumi mbele diamond platnumz angekua bosi wake, hakuna ambaye angekubali na wengi wangecheka. Tukubali tukatae, kwa sasa diamond platnumz ni mkubwa hata taifa linamuangalia. Mchango anao toa kupitia ajira ambalo ndio janga kuu la taifa, makapuni anayo endesha ninamini yana tija kubwa sana kwa taifa kupitia kodi anazo lipa lakini pia kwa huduma anazotoa.

Sasa wewe kijana na degree yako, unakwenda twitter kusambaza na kuchafua mtanzania mwenzio ambaye katumia akili binafsi na juhudi binafsi kujiweka alipo. Kuna watu wapo twitter na kwingine wanatumia degree zao kuunga mkono vitu kama hivi. NI UJINGA. Labda tu nikukumbushe ndugu; Umekwenda chuo kikuu, inawezekana umesoma kwa boom, tulitarajia uje mtaani baada ya masomo yako uwe ‘DIAMOND PLATNUMZ’, uoneshe na uwe mfano wa nini maana ya kusoma. Sasa leo unatumia digirii yako kumvunja vunja kijana mwenzio alie fanya kile kinacho kushinda wewe na magamba yako. Sio sawa. usijaribu kujificha kwenye kivuli cha chuki kwa diamond platnumz, kubali kua kufeli kwako ni wewe na machagua yako katika maisha yako.

Diamond Platnumz hajui milango ya UDSM wala UDOM au CBE, lakini mambo anayo fanya ni mtu mwenye upeo mkubwa. Kama kuna mtu ana mmentor diamond basi ningependa kumjua. Lakini anadhihirisha kwamba Chuo Kikuu Cha Maisha Hasa Kiko Mtaani.

Vijana hasa wasanii tuache kufuata mikumbo, jambo kubwa kama hili si jambo la kuchukulia kirahisi, fikiri kwa mapana. Diamond Platnumz ama ashinde hii tuzo au asishinde; anahitaji sapoti ya watanzania wenzake. Kugawanyika na kumpinga hakuna madhara kwa diamond, tayari kisha jenga platforms na fan base kubwa sana ndani na nje ya nchi, mambo yake yatakwenda umchukie umkubali. Pekee atakacho kosa ni wewe kua si rafiki yake; lakini pesa ataendelea kupata. Jina lake litaendelea kukua. Swali kwako wewe unaye pambana na fan bez ya mbagala, temeke na kariakoo. Utafika wapi? au hii chuki isiyo misingi itakusaidia nini?

Ikumbukwe pia kwa Diamon Platnumz kufika alipo fika kuna watu waliweka pesa zao na muda. Tuheshimu.

Inspiration:
Kama mafanikio ya diamond platnumz hayakupi inspiration; basi inawezekana hauja mfuatilia kwa karibu au basi wewe ni hater. Sitaongelea yaliyo dhahiri, nitamuongelea mtoto kutoka Rwanda ambaye mpaka sasa duniani na miandaoni kumezaliwa #hashtag ya #karyuridance. Namuongelea mtoto huyu kwa sababu ni nyimbo za diamond platnumz kama Baba Lao na Iyope zimemfanya ajulikane na hata ikafikia hatua kapata msaada kutoka kwa msanii mkubwa nchini Rwanda Meddy. Youtube, Instagram na kwingineko huyu mtoto anatamba sana na ni maarufu kuliko mimi na wewe. Kwa sasa huyu mtoto yuko chini ya kituo cha watoto wenye vipaji Nyakanazi Kids Talents ambao pia wamemuona baada ya kupigwa kiki na makukato ya diamond platnumz, kituo hiki cha watoto kina ishi kwa mapato ya youtube pekee. Kituo hicho kinapata mamilioni ya views na inakadiriwa kinaingiza kati ya Mil 20 hadi 40 kwa mwezi.

Download Meddy yongeye gutungura The ben abantu barumirwa m

Wanasiasa:
Hili sitazungumza sana, lakini kwa haya yanayo endelea, wanasiasa wajifunze kitu. mpaka sasa wanasiasa wako kimya wako kwenye maofisi na V8s maisha yanasonga, huku diamond anapita kwenye makaa ya moto. Sisemi kwamba nibaya kwa msanii kushiriki kampeni za kisiasa, lakini inabidi waangalie vizuri namna ya kuwatumia. Waitwe kama watoa burudani na si sehemu ya kampeni kumnadi mtu flani. Kama kuna dau/pesa msanii analipwa kufanya show kwenye jukwaa la siasa basi iwekwe wazi kua ameitwa kufanywa show na ikiwezekena makubaliano yawe wazi amelipwa kiasi gani. Hii itahesabika ni kama dili la kibiashara, hakuna anaye kataa pesa.

Kwako Diamond Platnumz
Binafsi mpaka kuandika hivi najua unajua kua haoko peke yako, ni wantanzania na watu wengi wako nyumba yako, Mpaka ulipofika umepitia mengi na sitaki kuamini kwamba hili limekutigisha, ila limekupandisha darasa moja zaidi. Ukubwa jalala huu si msemo mpya kwako na kama ndio unasikia basi jua unamanisha yanayotokea. Kiongozi kupigwa mawe haimanishi anafanya vibaya, jua kwamba wanao kupiga mawe wanahitaji kuongozwa. Siku zote katika kutafuta mafanikio unaweza ukawa unashangiliwa na kupigiwa makofi na mtu mmoja au wawili tu, lakini ukifanikiwa unapigiwa makofi na hata usio wafahamu. Kaza buti mzee Baba, shikilia hapo hapo. Ulivyo anza pia ulibezwa. Ulipofanya colabo ya kwanza kimataifa ulibezwa. Wakasema wewe ndio unabebwa na hautafika popote. Leo imebaki stori.

Hapo zamani, Mwl. Nyerere aliya jua haya ndio mana Chama kilikua na bendi na msanii mwenye mvuto alikuwepo kama marehemu mzee Komba wa CCM Nambari One. Iliwezekana na hakukua na shida. Kwanini vyama kama vinaona kuna ulazima kua na burudani kisiasa, visiajiri bendi au wasanii kabisa ambao kazi yao ni mziki wa chama au siasa?

* UDAKU SPECIAL DAILY WAMEANDIKA HII HAPA CHINI NA GAZEEP TUMEIPENDA *

Niko Ulaya na nimeshuhudia popote panapopigwa muziki wa afropop basi ni Nigeria, South Africa, DRC na Tanzania, nikisema Tanzania basi ni muziki wa Diamond Platnumz au kundi zima la WASAFI.

Mwaka 2017 nilikuwa Nairobi na kwenda club ambapo nilishuhudia karibu 90% ya muziki uliokuwa unapigwa basi ulikuwa ni wa Diamond ama msanii wa kundi lake, wakizidi sana walikuwa wanapiga muziki wa Navy Kenzo “kamatia chini”.

Ni akili iliyojaa matope tu kujaribu kuzuia nyota wa pop wa Tanzania Diamond Platnumz eti asishinde tuzo za BET2021 eti kwa sababu aliiunga mkono CCM kwenye uchaguzi wa 2020.

Huyu kijana nyota licha ya kwamba ana kipaji ni mtu mwenye juhudi zisizo na mfano hasa ukichukulia kwamba anatoka nchi iliyojaa vijana wavivu wa kufikiri na wasio na juhudi ya kutafuta mali.

Diamond Platnumz ameajiri vijana wengi sana na hivyo kuboresha maisha ya watanzania wengi bila ya kujali itikadi zao.

Diamond ni mfanya biashara hivyo hachagui afanye kazi na nani, hata siku CHADEMA wakija na pesa ndefu kwa nini asimuimbie Mwenyekiti Mbowe, kamanda wetu asiyetetereka?

You may also like...