RUVU SHOOTING WANAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA

RUVU SHOOTING YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA
RUVU SHOOTING YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA

RAJAB Mohamed kocha msaidiz wa Ruvu Shooting amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwa nja wa Mkapa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari,  makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,  (TFF), Mohamed amesema kuwa maandalizi yapo tayari na wanahitaji pointi tatu muhimu. 

“Maandalizi yapo vizuri na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

“Wapinzani wetu Yanga tunawaheshimu na tunatambua kwamba ni timu kubwa lakini tupo tayari kwa kuwa mchezo wa Kwanza tulipokutana nao tulipoteza makosa tumeyafanyia kazi,” amesema.

Mchezo wao wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa,  ubao ulisoma Yanga 2-1 Ruvu Shooting hivyo kesho mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Kua wa kwanza kupata taarifa

You may also like...