RAIS WA BENKI YA AfDB AMUAHIDI RAIS SAMIA NEEMA LUKUKI KWA TANZANIA, NI KATIKA MAZUNGUMZO YAO KWA NJIA YA SIMU, LEO

RAIS WA BENKI YA AfDB AMUAHIDI RAIS SAMIA NEEMA LUKUKI KWA TANZANIA, NI KATIKA MAZUNGUMZO YAO KWA NJIA YA SIMU, LEO
RAIS WA BENKI YA AfDB AMUAHIDI RAIS SAMIA NEEMA LUKUKI KWA TANZANIA, NI KATIKA MAZUNGUMZO YAO KWA NJIA YA SIMU, LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza kwa njia ya simu masuala mbalimbali ya Kimaendeleo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dk. Adesina Akinwumi, ambaye alikuwa akizungumza kutokea Makao Makuu ya Benki hiyo Abidjan nchi Ivory Coast leo, Ijumaa, Juni 11,  2021. 

Ikulu, Dar es Salaam, leo
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Adesina Akinumwi, amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa Benki hiyo itaendelea kufadhili miradi ya maendeleo hapa nchini na ipo tayari kufadhili miradi mipya kwa kuwa Tanzania ina sifa za kuendelea kupata ufadhili.

Dk. Adesina amesema hayo leo, akiwa mjini Abdjan nchini Ivory Coast, wakati akizungumza kwa njia simu na Rais Samia akiwa Ikulu, Jijini Dar es Salaam, kuhusu uhusiano wa Tanzania na Benki hiyo ambayo imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiloano ya Rais, Ikulu, Jafar Haniu, imesema, katika mazungumzo hayo Dk. Adesina alianza kwa kutoa pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dk. John Magufuli na kumpongeza Rais Samia kwa kupokea kijiti cha Urais.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kisha Dk. Adesina akasema Tanzania inafanya vizuri katika uchumi na ana matumaini makubwa kuwa Rais Samia ataendeleza jitihada zilizokuwa zikifanywa na mtangulizi wake.

Dk. Adesina ameahidi kuwa AfDB itatoa ufadhili kwa Tanzania ili kuanzisha Benki za Wajasiriamali zitakazowakopesha vijana wanaohitimu mafunzo ya ufundi stadi pamoja na kujihusisha na kilimo, jambo litakalosaidia kupungua kwa tatizo la ajira kwa vijana na kuwaongezea kipato.

“Aidha, Dk. Adesina amemualika Rais Samia kuhudhuria mkutano wa uwekezaji utakaowaleta wawekezaji wakubwa pamoja ambao unatarajiwa kuvutia mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuwekeza katika nchi mbalimbali.

Pia, Dkt. Adesina amesema AfDB imetenga Dola Bilioni 5 za Marekani kwa ajili ya kusaidia wanawake na ameomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa uwezeshaji wanawake kiuchumi ambapo Rais Samia amekubali ombi hilo”, amesema Haniu katika Taarifa hiyo.

Haniu amesema katika taarifa hiyo kuwa pia Dk. Adesina ameahidi kuleta wataalamu wa Benki hiyo hapa nchini ili wakutane na wataalamu wa Tanzania kwa ajili ya kupitia miradi ambayo tayari inafadhiliwa na benki hiyo na kujadili fursa za kuanzisha miradi mipya.

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Dk. Adesina kwa salamu zake za pole na pongezi na amemshukuru kwa benki hiyo kufadhili miradi mingi ya maendeleo hapa nchini ikiwemo inayotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa awamu ya pili na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na benki hiyo.

“Rais Samia, ameelezea kufurahishwa kwake na mradi wa AfDB wa kufadhili vijana wanaojihusisha na kilimo na wanaomaliza mafunzo katika vyuo vya ufundi stadi kwa kuwa ufadhili huo utawawezesha vijana wengi wa Tanzania kuzalisha mali.

Pamoja na kumpongeza Dk. Adesina kwa ushindi wake wa kuchaguliwa kuwa Rais wa AfDB kwa kipindi cha pili, Rais Samia amemuomba kuongeza nafasi za Watanzania wanaoajiriwa katika benki hiyo”, imesema taarifa hiyo.

Kua wa kwanza kupata taarifa

You may also like...