RC KUNENGE AZINDUA MAGARI YA HONGYANG KATIKA KIWANDA CHA GF KIBAHA, AKEMEA WATENDAJI WANAOWATIA HOFU WAWEKEZAJI

RC KUNENGE AZINDUA MAGARI YA HONGYANG KATIKA KIWANDA CHA GF, AKEMEA WATENDAJI WANAOWATIA HOFU WAWEKEZAJI
RC KUNENGE AZINDUA MAGARI YA HONGYANG KATIKA KIWANDA CHA GF, AKEMEA WATENDAJI WANAOWATIA HOFU WAWEKEZAJI

Kibaha, Pwani

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amezindua awamu ya  pili ya utengenezaji wa magari aina ya Hongyang katika Kiwanda cha magari cha GF Assemblers cha Kibaha mkoni Pwani.

Akizungumza baada ya uzinduzi wa magari hayo leo Kiwandani hapo, Kibaha mkoani Pwani, RC Kunenge amekemea baadhi ya tabia za Watendaji wa Serikali za kupishana katika ofisi za wawekezaji kwa visingizio mbali mbali.

Kunenge amevitaja baadhi ya visingizio baadhi ya Watendaji ha wa Serikali kuwa ni pamoja na kulazimisha kuonana na wamiliki au kuzingizia kutaka kufanya ukaguzi  hali inayowafanya wawekezaji kuwa na hofu na hivyo kushindwa kutimiza majukumu yao vizuri.

Kunenge amesema Serikali ya mkoa wa Pwani chini yake inahakikisha inapata maendeleo kwa kuongeza fursa ya biashara na uwekezaji wenye mazingira rafiki na utawala bora kwa hivyo hataki kusikia au kuona watendaji wanakua kikwazo katika kufanikisha mpango huo na kwamba hatawavumilia.

“Wakati Serikali ikijenga mazingira rafiki na wawekezaji sisi wenyewe maafisa wa Serikali tumekuwa kikwazo, hii haikubaliki”, amesema Kunenge.

Nae Meneja wa kampuni  GF Vehicle Assemblers , Ezra Mereng amesema lengo Kampuni hiyo ni kuunda kila aina ya chapa (brand ) ya magari kwa kuwa teknolojia na mitambo waliyonayo inauwezo wa kuunganisha magari aina zote kwa viwango na vigezo vya Kitaifa na kimataifa. 

Mereng amesema kiwanda hicho kilianza kwa kuunda magari chapa ya FAW na sasa  wamezindua  chapa nyingine  ya Hongyang na kuwataka wadau na Kampuni zingine  za magari kuacha kuagiza nje ya nchi badala yake wapeleke GFA kuundiwa (Assembling) kwa kuzingatia vigezo vyote vya kimataifa.

Kua wa kwanza kupata taarifa

You may also like...